Lipuli wameandikia barua TFF kuwathibitishia kwamba Simba SC wamefuata na kukamilisha taratibu za usajili wa Kwasi na sasa wamerishia uhamisho huo.
Awali, Lipuli iligoma kumruhusu Kwasi kwenda Simba baada ya timu ya Dar es Salaam kutofuata taratibu za kumhamisha.
Kwasi anakwenda kuchukua nafasi ya Mzimbabwe, beki wa kati, Method Mwanjali ambaye ameachwa kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe.
Poppe,
Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba
katika dirisha hili dogo Simba imeacha na kusajili mchezaji mmoja mmoja
tu wa kigeni ili kuimarisha kikosi chake.
Kwasi anaondoka Lipuli baada ya miezi mitano ya kuchezea timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu tangu ajiunge nayo kutoka Mbao FC ya Mwanza.
No comments:
Post a Comment