
Mzee huyo ambaye ni mkaazi wa Jadida anakabiliwa na
kosa la kushambhulia kwa aibu mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mtatu na nusu
, ametakiwa kuweka fedha taslimu shilingi milioni tatu na nusu .
Aidha masharti mengine ya dhamana ni kuwa na wadhamini
wawili kwa kila mmoja shilingi milioni mbili za maandishi .
Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali
Mohammed Ali mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya kuwa
mtuhumiwa ametenda kosa hilo tahere 13/12/2017 majira ya tano za asubuhi.
Mtuhumiwa huyo amekana kutenda kosa hilo , ambapo
ameiomba mahakama impe dhamana ombi ambalo limekubaliwa lakini ameshindwa
kutumiza masharti ya dhamana na kupelekwa ryumande hadi tarehe 8/2/2018
No comments:
Post a Comment