 |
Waandishi wa Habari wakifuatilia Mafunzo ya Kuwajengea uwezo wa kuandaa taarifa na habari bora za vipindi vya Redio |
Waandishi wa habari
nchini wametakiwa kuandika habari zenye kuibua
changamoto zinazowalenga wanawake katika jamii ili kuzitafutia ufumbuzi pamoja
na kudai haki zao.
Akiwasilisha mada
kwenye mafunzo ya uandaaji vipindi na kuwajengea uwezo waandishi wa habari yanayoendelea
mkoani Dodoma, Mwezeshaji kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni – UNESCO- BI ROSE MWALIMU amesema kuwa, bado wanawake nchini hawajapewa
kipaumbele katika kupaza sauti zao jambo ambalo linawafanya kubaki nyuma
kimaendeleo.
Bi Rose amesema
kuwa ni asilimia 22 tu ya idadi ya wanawake ndio wanaoshirikishwa katika taarifa
za habari ikilinganishwa na wanaume ambao ushiriki wao ni mkubwa .
 |
Waandishi wa Habari wakifuatilia Mafunzo ya Kuwajengea uwezo wa kuandaa taarifa na habari bora za vipindi vya Redioyanayoendelea Mkoani DODOMA |

(PICHA ZOTE NA GASPARY CHARLES.. MICHEWENI RADIO)
No comments:
Post a Comment