DC MICHEWENI: Wananchi Wahamasishwe Kujitokeza Siku ya Maadhimisho ya UKIMWI Duniani
MICHEWENI
Mkuu wa wilaya ya Micheweni Salama
Mbaruku Khatib amewataka watendaji mbalimbali wa wilaya humo kutoa mashirikiano
ya kutosha katika hafla ya kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yanakayofanyika
Desemba mosi ya kila mwaka.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa rai hiyo
katika kikao cha maandalizi ya hafla hiyo dhidi ya watendaji kutoka taasisi
mbalimbali, wakiwemo masheha kwenye ukumbi wa mikutano wa Zangoki wilayani
hapo.
Amesema kuwa katika kuhakikisha zoezi
hilo linakamilika kwa ufanisi ni lazima kila mtendaji kujitoa ipasavyo kwani
siku hiyo imetengwa kimataifa kwa ajiri ya zoezi hilo.
Aidha katika hatua nyingine Salama
amewataka masheha wa wilaya ya Micheweni kuhamasisha wananchi wao kujitokeza kwa wingi kushiriki
katika hafla hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
halimashauri ya wilaya ya Micheweni Hamad Mbwana Shehe, amesema kuwa
ameridhishwa na juhudi zinazofanywa na Mkuu huyo wa wilaya kwa kushirikiana na
watendaji mbalimbali katika masuala ya maendeleo.
Nae Sheha wa Shehia ya Micheweni Mjini ambae
pia ni mwenyekiti wa Masheha wilayani humo, Dawa Juma Mshindo, amemhakikishia
mkuu huyo wa wilaya kuwa watashirikiana nae katika kuhakikisha zoezi hilo
hilakamilika kikamilifu.
Siku ya UKIMWI Dunia ambayo huadhimishwa
kila ifikapo Desemba mosi ya kila mwaka,
katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Maadhimisho hayo yanatarajia
kufanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Micheweni huku Mgeni rasmi
akitarajiwa kuwa mkuu wa Wilaya hiyo Bi Salama Mbaruk Khatib.
Post a Comment