Naibu Waziri SHAMATA: Asijitokeze Afisa Afya Yoyote Kutaka Kuingiza Mkono Kwenye Kesi za Udhalilishaji
Baadhi ya Maofisa hao Wakijitambulisha Kabla ya Kikao hicho kuanza |
Afisa Mdhamini Wizara ya \Nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na idara maalum SMZ, Juma Nyasa, akizungumza katika kikao hicho kabla ya kufungwa |
Gari la Naibu waziri wizara ya nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na idara maalum SMZ, Shamata Shaame Hamis likiwa limepaki Nje ya ukumbi wa Halimashauri ya Wilaya ya Micheweni |
Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum SMZ, Shamata Shaame Hamis amewataka wakuu wa vituo vya afya Wilaya ya Michewni kutoa ushirikiano zaidin linapotokea suala la udhalilishaji.
Akizungumza katika kikao na maofisa afya, kilimo, mifugo, misitu na uvuvi katika ukumbi wa halimashauri ya wilaya ya Micheweni amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale maofisa watakao jitokeza kutaka kukwamisha mapambano dhidi ya udhalilishaji.
Naibu waziri, Hamis amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya maofisa afya wamekuwa kikwazo cha kumpambana na udhalilishaji kwa kushindwa kutoa taarifa za vipimo sahihi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Micheweni Salama Mbaruk Khatib, amewataka maofisa afya kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi kwa kutumia lugha nzuri kulingana na maadili ya kazi zao.
Aidha katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya amewataka maofisa hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kuzingatia mipango kazi yao kama inavyo waelekeza.
Kikao hicho cha Naibu waziri wizara ya nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na idara maalum SMZ, Shamata Shaame Hamis ni mwendelezo wa ziara yake kikazi Wilaya ya Micheweni katika kujadiliana na maofisa wa idara mbalimbali juu ya utendaji kazi wa mpango wa ugatuzi wa Madaraka kutoka serikali kuu mpaka serikali za mitaa.
Post a Comment