RC KAS PEMBA: Washirikisheni Walemavu Katika Kazi za Maendeleo
Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba mhe omar khamis Othman ameitaka jamii kuacha kuwaficha majumbani watu wenye ulemavu bali iwashirikishe katika kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo katika maeneo yao .
Mh Omar ameyasema hayo huko katika ukumbi wa Jamhuri Wete wakati akifungua mkutano wa siku moja uliowashirikisha masheha wenye lengo la kupata uelewa wa zoezi la usajili wa watu wenywe ulemavu.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na katibu tawala Mkoa wa huo Ahmed Khalid Abdalla, amesema usajili wa watu wenye ulemavu unakwenda sambamba na haki za binadamu.
Aidha amefahamisha kwamba kitendo cha kuwaficha watu wenye ulemavu kinawanyima fursa ya kushiriki katika vikao vya maamuzi jambo ambalo linawakosesha haki ya ushirikishwaji ndani ya jamii.
Mapema Mkurugenzi Idara ya watu wenye ulemavu Zanzibar Abeida Rashid Abdalla amesema lengo la zoezi hilo ni kuwafichua watu wenye ulemavu ili waweze kutambulika na kupata haki zao za msingi
Akizungmza katika kikao hicho mratibu kutoka Idara ya watu wenye ulemavu Pemba Mashavu Mabrouk amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili walemavu ni kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji
Post a Comment