Msitu wa Uluguru Watoa Neema kwa wakazi wanao uzunguka
WAKAZI wa vijiji 62 vinavyozunguka hifadhi ya msitu Asili Uluguru mkoani Morogoro , wameanza kunufaika na mafunzo ya shughuli mbadala ambazo zitawafanya wasiitegemee hifadhi hiyo kwa ajili ya mahitaji yao.
Afisa misitu wa hifadhi hiyo Mohammed Adam Borry amesema mafunzo hayo kwa wanavijiji hao yanalenga kudhibiti uharibifu ndani ya hifadhi hiyo .
Borry amewaambia wandishi wa habari waliokuwa kwenye mafunzo ya uwandishi wa habari za Mazingira , baada ya kutembelea hifadhi hiyo kuwa , mafunzo hayo ni ya kupanda miti ya muda mfupi ya matunda na mbao .
Amesema , wakazi wa vijiji hivyo wameanzisha kilimo cha magimbi , ndizi pamoja na shughuli za ufugaji wa nyuki ambazo zimesaidia kuimarisha hali ya uhifadhi wa mazingira .
“Uvamizi katika hifadhi hii umepungua ni baada ya wakazi wa vijiji hivyo kupatiwa mafunzo ya shughuli mbadala za kujipatia kipato na kuwafanya wasitegee hifadhi kuendesha maisha yao ”alisema Borry.
Aidha Borry amesema ushirikiano wanaupata kutoka kwa wakazi wa vijiji hivyo , ambao wanashirikiana na watendaji wa Hifadhi kufanya doria na kwamba kila kijiji kimeunda kamati ya maadili ya kudhibiti uharibifu.
“Hakuna uvanaji wa miti ndani ya hifadhi , hii inatokana na ushirikiano uliopo kati ya watendaji wa hifadhi na wanakijiji ambao wameunda kamati za maadili , kwa kweli tunawashukuur sana wanavijiji ”alieleza.
Hata hivyo wandishi wa habari wameushauri uongozi wa Hifadhi hiyo kuandaa utaratibu wa kuwapatia motisho wanavijiji hao , ili kuwafanya wasijihusishe na vitendo vya hujuma ndani ya hifadhi .
Abeid Said Dogoli kutoka Abood Media Company ameshauri fedha ambazo zinapatikana kuwepo na utaratubu wa kuwagaiwiya wanavijiji hao ili kuwapa moyo wa kuendeleza ushirikiano wa udhibiti wa vitendo vya uharibifu .
Mafunzo hayo ya siku tano kwa wandishi wa Habari za Mazingira yameandaliwa na Muungano w a Vilabu vya wandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia vilabu wa wandishi wa habari za Mikoa na kupata ufadhili kutoka Ubalozi wa Sweeden nchini Tanzania .
Na Masanja Mabula
Post a Comment