Rais DK. SHEIN: Wala Rushwa ndani ya CCM lazima Wajadiliwe
VIJANA wa Chipukizi wakimvisha sikafu Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika mapokezi yake. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla Mabodi(kushoto) akibadilisha mawazo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika hafla hiyo |
BAADHI ya wanachama wa chama cha Mapinduzi walioudhuria katika hafla hiyo. |
Katibu msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Daud Ismail Juma akisoma risala ya Wana CCM wa Mikoa Sita kichama Zanzibar. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla Mabodi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo. |
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib akizungumza kwa niaba ya Wana CCM wa Mkoa huo |
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM), Mwekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka
viongozi wa chama kutosita kuwajadili wanachama ambao wanakiuka maadili ya chama
hususan vitendo vya rushwa.
Pia, amesema wanachama hao
wakishajadiliwa hawatasita kufukuzwa ndani ya CCM na kwamba imefikia hatua
baadhi ya watu hao ambao wanafanya vitendo hivyo wanaonewa haya.
Hayo ameyasema leo , katika
sherehe za kumpongeza kuchaguliwa tena nafasi ya Makamu Mwenyekiti, iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa Mjini ,ambapo aliwataka viongozi hao
kutofumbia macho vitendo hivyo ndani ya CCM.
katika maongezi yake Dk.Shein
ameongeza kuwa vitendo hivyo vya rushwa si jambo jipya ndani ya CCM na kwamba
inaharibu sana maadili ya chama.
"Vitendo hivi vya rushwa
ndani ya CCM si suala jipya lakini tunaoneana huruma, tunafichiana na baadae
tunalalamikiana wakati chama ni ya wanachama hivyo lazima
tushirikiane,"amesema.
Makamu Mwenyekiti huyo Dk.Shein
amesema utaratibu wa chama kinajielekeza wanachama ambao wanakiuka maadili
wanapaswa kujadiliwa kuanzia ngazi za tawi na baadae inawasilishwa kwenye
uongozi wa juu na kuchukuliwa hatua.
Ameeleza chama kipo kwa
wanachama ikiwemo kwenye mashina na matawi na taratibu zinafafanua kuwa ngazi
hizo ndipo mambo hayo yanazungumzwa kwamba mwanachama akikiuka maadili
anajadiliwa kwenye tawi.
"Anajadiliwa kwenye kamati
ya tawi na shina, kamati ya jimbo, kamati ya wilaya, Halmashauri ya wilaya
ndipo wanapojadiliwa huku kwamba anafaa ama hafai hachukuliwe hatua za
kufukuzwa ama asichukuliwe,"amesema.
Makamu Mwenyekiti huyo amesema
utaratibu unaeleza kuwa baada ya kujadiliwa wanachama hao taarifa itapelekwa
kwenye ngazi za juu na kufanya maamuzi ya kumfukuza.
"Nachotaka kueleza kuwa
kazi hii ni ya wote na kwamba jukumu kubwa ni kuhakikisha CCM inashinda mwaka
2020 msiwafiche watu ambao wanataka kuharibu chama, na kwa kufanya hivyo ni
sawa na kuwa ndumi la kuhili tunayoyasema sio tunayoyafanya,"amesema
Makamu Mwenyekiti.
Amefafanua kuwa kazi ya siasa
ya kipindi hiki lazima kuongeza kasi ambapo kuna mambo zaidi ya kuyafanya na
hata Mwenyekiti Dk.John Magufuli alisisitiza kwenye mkutano mkuu uliofanyika
Desemba 18, mwaka huu mjini Dodoma.
Mbali na hilo, Dk.Shein
amewataka viongozi wa serikali kutambua na kuheshimu CCM kutokana na kuwa
wanafanya kazi ya utekelezaji wa chama hivyo hawanabudi kukithamni.
Kwa upande wake Naibu Katibu
Mkuu Zanzibar, Dk.Abdallah Juma Saadalla(Mabodi), amesema wanachama kutoka
visiwani humo wanatarajia kusimamia vyema ibara ya tano ya kuhakikisha CCM
inashinda mwaka 2020.
Ameongeza kuwa uchaguzi
uliopita ulikuwa na mawimbi makubwa sana lakini watu walioshiriki walikuwa
wanastahili.
"Bado tunafanya juhudi za
kutoa elimu kwa viongozi wa chama kuhusu suala la kuzingatia kanuni na maadili
ili kuhakikisha wanasongesha gurudu la uchaguzi wa mwaka 2020"amesema.
Dk.Mabodi ameeleza kuwa
anamshukuru Mungu kwa kuwa wagombea wote ambao wamepita kwenye uchaguzi huo
asilimia kubwa wana maadili ya kutosha.
Post a Comment