SOS kuleta miundo mbinu kwa baadhi ya skuli katika wilaya ya micheweni.
afisa elimu wilaya ya micheweni mwalimu mbwana shaame akizungumzia juu ya wazazi kushirikiana na walimu kwa maendeleo ya watoto hapo jana katika ukumbi wa skuli ya micheweni sekondari. |
afisa mradi kutoka SOS Gharibu Abdalla Hamad akizungumzia juu ya shirika hilo kuboresha baadhi ya skuli na kuleta maendeleo bora. |
wazazi na walimu wakisikiliza ahadi mbalimbali kutoka kwa SOS katika kuzisaidia skuli ambazo hazina miundo mbinu ya kutosha. |
wazazi akisikiliza takuwimu za watoto wao kutoka kwa afisa wa elimu wa wilaya ya micheweni juu ya ufaulu wa watoto wao. |
wazazi na walimu wakitoa changamoto zao kwa SOS na kwataka kuzisaidia skuli ambazo hazina miundo mbinu ya kutosha. |
Shirika la
kusaidia kaya masikini zanzibari SOS limewataka wazazi,kamati za skuli na
walimu wakuu wa skuli zilizopo wilaya ya Micheweni kusimamimia vyema watoto ili
kupata elimu ikiwa ni haki yao ya msingi.
Kauli hiyo ilitolewa
na afsa mradi kutoka shirika hilo, Gharibu Abdalla Hamadi wakati alipokuwa
akizungumza na walimu pamoja na kamati zake katika ukumbi wa mikutano skuli ya
sekondari Micheweni.
Alisema mradi
umelenga kuboresha katika upatikanaji wa vyoo kwa baadhi ya skuli zilizomo
ndani ya wilaya ya Micheweni pamoja na kujenga majengo ya kisasa yatakayokidhi
haja za wanafunzi.
“kwa mwaka huu SOS
itaweka maboresho kwanza kwenye vyoo kwa baadhi ya skuli kama vile Kiuyu Na
Tumbe ili wanafunzi kuepuka kwenda vichakani kwaajili ya kufanya haja zao,” Gharibu
alisema.
Gharibu aliwataka
wazazi kuwasomesha watoto wao walio kwama kimasomo na kuwapeleka katika vyuo
vyo kiufundi kwaajili ya kupata ujuzi utakao waendeleza kimaendeleo.
“wazazi ni
kuwatafutia njia mbadala watoto wenu walio kwama kimasomo na kuwapeleka katika
vyuo vya kiufundi kwa kupata taaluma mbalimbali kwa ajili ya kujiendeleza
kimaendeleo na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana” Gharibu alisema.
Hata hivyo afsa
elimu wilaya ya Micheweni Mbwana Shame alisema elimu ni haki ya kila mtu hivyo
ni vyema wazazi, walimu na kamati za skuli
kushirikiana ili kusimamia vyema maendeleo ya watotot wao.
Mbwana alisema ni lazima wazazi kuchukuwa
juhudi za kuwatembelea watoto mara kwa mara katika skuli zao, ili kujua
changamoto mbalimbali zilizopo katika maendeleo ya watoto wao na kupata njia
muafaka ya kutatua changamoto hizo.
“wazazi
ni vyema kuwatembelea watoto sio kuwapeleka skuli ndio kusoma kwani inawezekana
ikawa hata skuli wenyewe hafiki lakini utakapo chukua juhudi ya kumtembelea
ndipo utakapo jua ni changamoto gani inayo mkabili mtoto wako na kujua nijinsi
gani ya kuondoa changamoto hiyo,” alisema.
Alisema kuwa
wazazi, walimu pamoja na kamati za skuli waweke mikakati na kanuni mbalimbali na kutoa hukumu
kwa wazazi ambao hawasimamii maendeleo ya watoto wao na kuifikisha kwa mkuu wa
wilaya kwaajili ya kutiwa saini na kupitishwa kanuni hiyo.
“wazazi ,kamati
pamoja na walimu mutakapokaa na kuandaa mipongo kazi yenu na kuifikisha kwa
mkuu wa wilaya na kutiwa saini basi wale wazazi ambao hawafuatilii maendeleo ya
watoto wao, watakua na tahadhari kubwa juu ya suala la kuangalia maendeleo ya
watoto wao,” mbwana alisema.
Washiriki wa
semina hiyo wamesema changamoto kubwa inayowafanya watoto kushindwa kwenda
skuli ni kujiingiza katika ajira za utotoni, hivyo wamewataka wazazi kuwa
karibu na watoto wao ili waweze kwenda skuli.
Na Omar Khamis Kombo
Post a Comment