DC WETE Aagiza Kufanyiwa Ukarabati Barabara ya Kinazini
Mkuu wa
wilaya ya WETE, ABEID JUMA ALI ameiagiza Wizara ya Ujenzi , Miundombinu na Usafirishaji
PEMBA kuifayia ukarabati Barabara ya Kinazini Shehia ya Mtambwe kusini ili
kunusuru madhara kwa wananchi.
Mkuu
wa wilaya amelazimika kutoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kutembelea eneo
la barabara hiyo na kuiagiza Wizara husika kuharakisha matengenezo ya Barabara
katika kabla ya mvua za masika.
Amesema Barabara
hiyo ambayo ni kiunganishi kwa wakaazi wa Shehia hiyo na maeneo mengine katika
kuyafikia masoko ya bidhaa , inahitaji ukarabati wa haraka ili wananchi
waweze kuitumia kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.
Nae
msimamizi mkuu wa Barabara Wilaya ya WETE, MASOUD ALI MUSA, amesema yuko tayari
kutekeleza agizo hilo kwa hatua ya mwanzo wataleta kifusi pamoja na mawe na
kulifukia kwa ajili ya kunusuru madhara hayo.
Barabara ya
kinazini Mtambwe ni miongoni mwa barabara ambazo zimeathirika na mvua kubwa
zilizonyesha mwaka jana.
Post a Comment