MZEE AKILIMALI - CHIRWA ASIWE ANAPIGA PENALTI ZETU..HANA BAHATI HATA KIDOGO
KATIBU
wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, amelitaka benchi la
ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mzambia, George Lwandamina, kuhakikisha
wanatafuta mbadala wa mchezaji atakayekuwa anapiga penalti badala ya Mzambia,
Obrey Chirwa.
Mzee
Akilimali ameyasema hayo kufuatia mshambuliaji huyo kuwa na mfululizo wa kukosa
penalti ambapo juzi Jumamosi alikosa tena wakati Yanga iliposhinda bao 1-0
dhidi ya St Louis katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar.
Kwa
mwaka huu, Chirwa amepiga jumla ya penalti tano ambapo kati ya hizo kakosa nne
dhidi ya URA kwenye Kombe la Mapinduzi, Ihefu katika Kombe la FA, Njombe Mji
kwenye Ligi Kuu Bara na St Louis. Aliyopata ni dhidi ya Ihefu ambapo kwenye mchezo
huo alipiga penalti mbili.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Mzee Akilimali alisema kuwa kwa upande wake analitupia
lawama benchi la ufundi la timu hiyo kwa kuendelea kumpa penalti mchezaji huyo
licha ya kutokuwa na bahati nazo hali inayowafanya kupata wakati mgumu kupata
matokeo.
“Kwangu
siwezi kumlaumu Chirwa hata kidogo, wa kulaumiwa ni benchi zima la ufundi
likiongozwa na Lwandamina kwa sababu sioni haja ya kuendelea kumtumia penalti
aendelee kupiga mchezaji huyo maana hana bahati nazo hata kidogo.
“Siku
zote amekuwa akikosa penalti katika michezo muhimu na hii ni (mechi) ya tatu
kwake lakini bado amekuwa akikosa, sasa kwa nini wasibadilishe na ukiangalia
katika mchezo wa jana (juzi) yeye ndiyo ameigharimu timu kwa kiasi kikubwa
lakini walimu sijui hawakuliona hilo au vipi,” alisema Mzee Akilimali.
SOURCE:hajimanara.com
Post a Comment