Header Ads

Uteuzi Mpya wa Viongozi SMZ



Image result for ALI SHEIN 

RAIS wa Zanzibar na MwenyekitiwaBaraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. ALI MOHAMED SHEIN amefanya uteuzi na kuwabadilisha nafasi baadhi ya viongozi katikaTaasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-
1. UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA
i. Bwana Issa Juma Ali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Pemba.
ii. Bwana Rajab Ali Rajab ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.

2. UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA WILAYA
i. Bwana Bakari Ali Bakari ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Kaskazini, Pemba.
ii. Bibi Fatma Mohamed Juma ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Kusini, Unguja.
iii. Bwana Juma Abdulla Hamad ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mjini.
iv. Bwana Hamza Mahmoud Ibrahim ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Magharibi B.
v. Bwana Makame Machano Haji ameteuliwa kuwa Katibu Tawalawa Kaskazini B.

3. UTEUZI WA OFISA MDHAMINI WA WIZARA YA AFYA – PEMBA
i. Bibi Shadya Shaaban Seif ameteuliwa kuwa Ofisa Mdhaminiwa Wizara ya Afya – Pemba.

4. UTEUZI WA MWENYEKITI NA MKURUGENZI MKUU WA WAKALA WA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO NA VYA KATI
i. Bwana Mussa Ame Silima ameteuliwa kuwa Mweyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati.
ii. Bwana AbdulhamidIdrisa Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati.

5. UTEUZI WA MKURUGENZI WA TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Dr. Mustafa Ali Garu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia.

6. UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA MAJI (ZAWA)
Bwana Mussa Ramadhani Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Kuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).

7. UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI NA WATENDAJI WA WAKALA WA MATUKIO YA KIJAMII
i. Bwana Haji Machano ameteuliwa kuwa Mwenyekitiwa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.
ii. Dkt. Hussein Khamis Shaaban ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.
iii. Bwana Idrisa Shaaban Zaharan ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anaehusika na Usajili wa Mzanzibari Mkaazi na Wageni Wakaazi katika Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.
iv. Bwana Shaaban Ramadhan Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anaeshughulikia Usajili wa Vizazi, Vifo, NdoanaTalaka.

8. UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA PBZ
Bibi Kidawa Hamid Saleh ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodiya Wakurugenzi ya PBZ.
Uteuzi huo unaanza tarehe 1Machi, 2018.

No comments