CHOMBO CHENYE NAMBA YA USAJILI T0058 CHAKAMATWA NA KETE 560 ZA UNGA ZINAZODHANIWA KUA DAWA ZA KULEVYA
Pemba
JUMLA ya kete 560 za unga zinazodhaniwa kuwa ni dawa za
kulevya zimekamatwa na vikosi vya ulinzi na usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba
zilizokuwa zikiingizwa kutoka Mkoa wa Tanga .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba , kamishna
Msaidizi wa Polisi Haji Khamis Haji amesema kukamatwa na kete zimekamatwa
zikiwa katika chombo chenye jina la SIYASEMI kikiwa na namba za usajili T 0058.
Amesema vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo vinafanya kazi
kwa ushirikiano vilifanikiwa kukikamata chombo hicho baada ya kupokea taarifa
kutoka kwa wananchi ambao ni raia wema wakati kinajiandaa kuondoka katika
bandari ya Tanga .
“Tumefanikiwa kukamata chombo chenye jina la SIYASEMI kikiwa
na namba ya usajili T 0058 na baada ya kukipekua tulibaini kuwa kimebeba kete
560 z aunga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya heroin” alieleza.
Aidha kamanda wa Haji amewataka wananchi kujitokeza kutoa
ushirikiano na vyombo vya ulinzi ikiwa ni pamoja na kutoaa taafisa sahihi
sambamba na kwenda kutoa ushahidi katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakamani .
“Nawaomba sana wananchi waendelee kuviunga mkono harakati za
vikosi vya ulinzi katika kudhibiti uingizaji wa dawa za kulevya kwa kuhakikisha
wanatoa taarifa sahihi sambamba na kutoa
ushahidi wanapohitaji ”alisisitiza.
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kaskazini
Pemba Mhe Omar Khamis Othman ameviagiza vyombo vya ulinzi Mkoa huo kuimarisha
doria sehemu za madiko ili kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya.
Aidha ameliagiza jeshi la Polisi
kumkamata mahodha wa Chombo hicho ili aisaidie Serikali kuhakikisha mhusika na
unga huo anapatikana na kufikishwa mahakamani .
“Anzeni na nahodha wa chombo hichi
licha ya kwamba amesema hakuwemo kwenye safari , mchukueni ili asaidie kumtambua mwenye mzigo
huu kwani tumechoka kuona vijana wanaathirika na utumiaji wa dawa za kulevya ”alisema.
Kufuatia kufanikiwa kukamatwa unga
huo , Mkuu wa Mkoa amevipongeza vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo
vimefanikisha kukamatwa kwa mzigo ambao , kama ungafanikiwa kuingizwa hapa
nchini ungeleta athari kwa vijana.
Mwisho .
Post a Comment