MAHAKAMA ZATAKIWA KUJITATHMINI ILI KUTOA MAAMUZI SAHIHI NA YA HAKI KWA JAMII.
PEMBA…….
Mkuu wa wilaya ya mkoani Hemed
Suleiman Abdalla amewataka watendaji wa
mahakama kujitathmini katika
utendaji wao wa kazi kwa lengo la kutoa maamuzi sahihi
na ya haki kwa jamii.
Amesema jamii inategemea kupata maamuzi ya haki kwenye
chombo hicho , ambapo watendaji wake wanalazimika kujisafisha na kujiepusha na
aina yoyote ya udanganyifu au upendeleo.
Ameyasema hayo leo huko ukumbi wa kituo cha huduma za sheria
tawi la pemba alipokuwa akiyafungua mafunzo ya siku mbili ya haki za binadamu
kwa makadhi na wazee wa mahakama kisiwani pemba .
Amewataka watendaji hao kusimamia haki ipasavyo ili kuifanya
jamii kuwa na imani na chombo hicho ambapo pia amewatahadharisha viongozi mbali
mbali kujiepusha kuingilia maaamuzi ya mahkama.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amesisitiza taaluma ya sheria kusambazwa
kwa wananchi vijijini ili kuwa na uwezo wa kuielewa katiba ya nchi na kuepuka
matatizo yasiyo ya lazima.
Mapema mratibu wa kituo hicho tawi la pemba Fatma Khamisi Hemed amefahamisha kwamba
kituo hicho hakifungamani na upande wowote wa
siasa na kinatoa huduma za kisheria kwa taasisi na makundi mbalimbali ya
wananchi bila ya malipo.
Jumla ya mada sita zinazohusu haki za binadamu zitajadiliwa
kwenye mafunzo hayo ya siki mbili yaliyotayarishwa na kituo hicho
Post a Comment