Header Ads

CCM YAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JIMBO.



WILAYA YA MICHEWENI….

Wanachama wa chama cha mapinduzi ccm wametakiwa kuwa na umoja na mashirikiano ili kuweza kukiletea ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Ushauri huo umetolewa na mzee wa chama hicho Micheweni Ramadhan Shaibu Juma wakati wa kufungua mkutano wa kuwachagua viongozi wa chama katika jimbo la Micheweni.

Amesema kila kiongozi ana jukumu la kuwahamasisha wananchi kujiunga na chama cha ccm ili kuongeza nguvu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020  na kuwa na wanachama wengi wenye kuleta manufaa zaidi ndani ya chama hicho.

Akitoa matokeo katika uchaguzi huo mjumbe wa siasa wilaya ya chake Salama Mbaruku Khatibu amemtaja  Ali Khamis Mbwana kuwa mwenyekiti kwa kupata kura 36 na kumshinda mpizani  wake  Shaame Faki Omari aliepata kura  29.

Kwa upande wa katibu aliechukua nafasi hiyo ni Omari Mwinyi Suwedi na kumshinda mpizani wake Haji Faki Kombo kwa kupata kura 16.

Nafasi zilizokuwa zinagombaniwa katika uchaguzi huo ni wajumbe wa halimashauri kuu ya jimbo ,mkutano mkuu wa jimbo,mkutano mkuu wa wilaya pamoja na mkutano mkuu wa mkoa na katibu mwenezi.

Hata hiyo baada ya kuchaguliwa viongozi hao wametakiwa kuendelea kukiimarisha chama ili kiweze kuleta mabadiliko.

Salama amesema viongozi watakapokuwa makini katika chama wataweza kuleta mabadiliko makubwa na kuweza kuongeza wanachama wenye uwezo wa kukitetea sehemu yeyote ile.

No comments