KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA CHAZIDI KUTOA ELIMU KWA VIONGOZI NA JAMII.
Pemba.
Viongozi
wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na wanajamii, kisiwani pemba, wamesema
mafunzo ya haki za binadamu, waliopewa na kituo cha huduma za sheria tawi la
pemba, yamewapa uwelewa wa mambo mbali mbali ya kisheria, ikiwa ni pamoja na
kujua wajibu wao, ndani ya jamii.
Wakizungumza
kwenye mkutano wa tathimini uliofanyika kituo cha huduma za sheria mjini chake chake,wamesema
kabla ya kupewa mafunzo hayo, hawakuwa na uwelewa huo kwa jamii wanayoizunguka.
Wamesema,
kwa sasa wameshawaambia wafuasi wao kuwa, ushahidi wa mtoto, mtu mwenye ulemavu
wa kuzungumza na ushahidi wa kielektroniki, unakubalika mahakamani, jambo
ambalo awali hawakuwa wakilifahamu.
Sheha
wa shehia ya shumba vyamboni wilaya ya micheweni, time said omar, amesema
mafunzo hayo nae aliwafikishia wananchi wake, na sasa wapeta uwelewa wa mambo
mbali mbali ya kisheria.
Kwa upande wake kiongozi wa kanisa la katolic wete, bibi: anatolia
mtawa, amesema waumini wa kanisa lake, wanafahamu vyema maana na katiba na
sheria.
Amesema awali akidhani wajibu wake kanisani ni kuwaelezea wafuasi
wake, sheria na kanuni za imani ya dini yao, na masuala ya kisheria za nchi
hawana wajibu huo.
Akifungua
mkutano huo, afisa mipango wa kituo cha huduma za sheria zaznibar zlsc tawi la
pemba, khalfan amour mohamed, amesema kituo baada ya kutoa mafunzo, kinafanya
tathmini ili, ili kujiridhisha iwapo mafunzo walioyatoa yamepokelewa.
Amesema,
mkutano huo wa tathimini, utawapa dira kwa kujipanga vyema, kwa ajili ya
mafunzo mengine yajayo, ili yaweze kufikia lengo lililokusudiwa.
Nae
afisa ufuatiliaji na tathmini, kutoka kituo cha huduma za sheria zanzibar,
khatib mohamed khatib, amesema ni muhimu mara baada ya kukamilisha mradi,
kufanya tathimi ili kujua changamoto na mafanikio yaliofikiwa.
Amesema kituo, kinawaamini wadau wake mbali mbali wakiwemo
viongozi wa dini, viongozi wa shehia pamoja na asasi za kiraia, kutokana na
kuishi kwao karibu na jamii.
Hata
hivyo, afisa huyo amewataka wadau hao wa kituo cha huduma za sheria, kuendelea
kuwaelimisha wananchi, juu ya kutambua haki za wajibu wao, na wanapokwama,
wasisite kukitumia kituo cha huduma za sheria, kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Kituo
cha huduma za sheria zanzibar kwa sasa kimo katika mikutano yake ya tathimini,
kwa wadau wake mbali mbali, waliowapa elimu ya sheria na haki za bindamu kwa
kipindi cha miaka minne iliopita.
Post a Comment