UNICEF LAIMARISHA HUDUMA ZA USAFI WA MAZINGIRA KOJANI.
PEMBA
Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba mhe Omar Khamis
Othman amesema misaada inayotolewa na shirika la kuhudumia watoto
ulimwenguni (unicef ) imesaidia kuimarika kwa huduma za usafi wa mazingira na
kudhibiti magonjwa ya mripuko katika kisiwa cha kojani.
Akizungumza na ujumbe kutoka shirika hilo ukiongonzwa
na mwakilishi wake hata nchini bwana ren’e van dangen amesema ujenzi wa vyoo
vya kisasa katika kisiwa hicho umesaidia kuimarika hali ya usafi wa mazingira
kisiwani humo .
Amesema kabla ya ujenzi wa vyoo hivyo , kisiwani cha
kojani kiilikuwa kinara wa ugonjwa wa kipindupindu , ambapo tangu kuanza
kutumika wnanchi wamekuwa na elimu sahihi ya kutumia vyoo tofauti na miaka ya
nyuma.
Naye mwakilishi wa shirika la unicef tanzania bwana Ren’e
Van Dangen amesema shirika lake litaendelea kusaidia sekta mbali mbali za
maendeleo ikiwemo afya ili kujenga afya bora kwa watoto .
Ujembe huo pia umetembelea kisiwa cha kojani
kuangalia na kufuatilia maendeleo ya miradi ambayo imefadhiliwa na
shirika hilo ambapo wananchi wa kisiwa hicho wameliomba shirika hilo kuongeza
msaada wa ujenzi wa vyoo .
Post a Comment