MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA YAZIDI KUSHIKA KASI.
PEMBA .
Kijana Ali Hamad Salum (32) mkaazi
wa Selemu wete amehukumiwa kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 15 au
kulipa faini ya shilingi milioni 40 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa
kupatikana na madawa ya kulevya.
Hukumu hiyo imetolewa na
hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyopo Wete, Makame
Mshamba Simgeni.
Ilidaiwa Mahakamani hapo na
mwendesha mashtaka Mohamed Ali Juma kuwa Januari 28, mwaka 2015 majira ya saa
5:00 asubuhi huko kisauni wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba kijana
huyo alipatikana na furushi moja na nyongo nne za bhangi.
Kupatikana na madawa ya kulevya ni
kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria namba 9 ya mwaka 2009 kama
ilvyorekebishwa na na sheria namba 12 ya mwaka 2011 sheria ya kuzuia uingizaji
na utumiaji wa mwadawa ya kulevya sheria za Zanzibar.
Kabla ya kusoma hukumu hiyo kijana
huyo alipewa nafasi kuiomba mahakama ambapo aliomba mahakama hiyo isimpe adhabu
kwa kua hilo ni kosa lake na wakatati alipokamatwa alipigwa na bado hajapoa
hivyo kupelekwa chuo cha mafunzo kutamuathiri kiafya.
Hata hivyo ombi hilo limepingwa na
upande wa mashtaka na kuitaka mahakama kutoa adhabu kali kwani matendo hayo
yamekithiri ili iwe fundisho kwake na vijana wengne wenye tabia kama hizo
Kesi hiyo ilianzwa kusikilizwa kwa
mara ya kwanza Machi 11, mwaka 2015
Post a Comment