UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA RAIS WAANZA KUFANYIWA KAZI KASKAZINI PEMBA.
PEMBA.
Serikali
ya mkoa wa kaskazini pemba imeanza kutekeleza maagizo ya mhe rais wa
zanzibar kwa kugawa majukumu ya utekelezaji wa maagizo hayo kwa maofisa
wadhamini wa wizara na taasisi za serikali.
Akizungumza
katika kikao cha kutathmini ziara ya mhe rais katika mkoa huo , mkuu wa mkoa wa
kaskazini pemba mhe Omar Khamis Othman
amewataka kuwa wakweli na wawazi ili kuendana na kasi ya utendaji wa rais kwa kuhakikisha
maagizo hayo wanayafanyia kazi.
Amesema
kila wizara inapaswa kushiriki katika kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo
yaliyotolewa na rais wakati wa ziara yake mwezi uliopita katika mkoa huo.
Wakichangia
katika kikao baadhi ya maofisa wadhamini wamesema tayari wameanza kuyafanyia
kazi maagizo ya mhe rais kwa kufanya ziara na mikutano ya watendaji wa
taasisi zao.
Mapema
katibu tawala mkoa wa kaskazini pemba Ahmed Khalid Abdala amewapongeza maofisa
wadhamini kutokana na mchango wao uliofanikisha ziara ya mhe rais katika mkoa
huo .
Naye
mkuu wa wilaya ya wete Rashid Hadid Rashid amewasisitiza wakuu hao wa taasisi
kuhakikisha wanawajibika katika kutekeleza maagizo ya mhe rais kwa uwazi ili
wananchi wazidishe imani na serikali yao.
Post a Comment