WILAYA YA MKOANI YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MIRADI YA MWENGE.
PEMBA.
Mkuu wa wilaya ya mkoani Hemed Suleiman Abdallah ameeleza
kuridhishwa kwake juu ya hatua iliofikia kwa miradi
inayotegemewa kuzinduliwa na kuwekea mawe ya msingi katika mbio za
mwenge wa uhuru wilayani humo kwa mwaka huu.
Mkuu huyo wa wilaya ameyaeleza hayo huko
afisini kwake mara baada ya kumaliza ziara ya
kutembelea maeneo ya miradi yao.
Amesema pamoja na kuridhishwa huko pia iko
baadhi ya miradi inahitaji marekebisho madogo madogo,ambapo
amezitaka kamati husika kufanya marekebisho hayo kabla
ya tarehe 20 mwezi huu.
Miradi aliyoitembelea ni pamoja na nyumba ya
madakatari michenzani, soko la matunda na samaki kangani, msitu wa kuotesha
mikoko mwambe na banda la skuli ya sekondari kengeja.
Miradi mengine ni kiwanda
cha kufyetulia matufali kengeja, kisima cha maji safi na
salama mahuduthi, mradi wa ufugaji wa ngo’nbe wa maziwa mgagadu,
mradi wa kilimo mseto mgagadu na mradi wa ujenzi wa
nyumba ya bei nafuu chambani.
Katika tathmini hiyo pia mkuu huyo wa wilaya
amezungumzia suala la uokoaji wa zao la karafuu wilayani
humo, ambapo amewataka wazazi kutowaruhusu watoto wao hasa wa
kike kushiriki katika uokotaji wa mpeta .
Aidha mkuu huyo wa wilaya ameitaka jamii
kushirikiana na waalimu juu ya ushibiti wa utoro wa wanafunzi
maskulini katika kipindi hichi cha uokoaji wa zao la
karafuu.
Post a Comment