MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA YAZIDI KUSHIKA KASI.
PEMBA.
Katika mwendelezo wa operasheni wa utokomezaji wa
madawa ya kulevya wa Jeshi la Polisi nchini hatimae Jeshi hilo mkoa wa Kusini
Pemba jana limefanikiwa kumkamata kijana mwengine akiwa na jumla ya kete
241 zinazodhaniwa kua ni madawa ya kulevya.
Akizungumza
na redio jamii kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amemtaja
kijana waliyemkamata kuwa ni Haji Balozi
Hassan (35) ambae alikuwa kwenye gari ya abiria akitokea mkoani
kuelekea micheweni.
Amesema
askari walimtilia mashaka abiria huyo ndipo walipoamua kumpekua na kufanikiwa
kumkamata na madawa hayo aliyokua nayo katika mifuko yake ya suruali.
Kamanda
Shekhan ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili kufanikisha
kutokomeza madawa ya kulevya yanayoonekana kuwa ni tatizo katika jamii.
Tukio
la kukamatwa Hassan ni tukio mfululizo wa watuhumiwa wa madawa hayo
kukamatwa kisiwani Pemba ambapo juzi Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia
mikononi mwanamke mmoja mkaazi wa Wete akiwa na kete 3621 zinazodhaniwa kuwa ni
madawa ya kulevya katika maeneo ya mbuguani Mkoani.
Post a Comment