DC Micheweni: Halmashauri Fanyeni Kazi kwa Kushirikiana na Wizara Ya Ardhi Kutekeleza Majukumu yenu
MKUU WA
WILAYA YA MICHEWENI SALAMA MBAROUK KHATIB AMEIOMBA HALMASHAURI YA WILAYA YA MICHEWENI KUSIMAMIA
UPIMAJI WA ENEO LINALOTARAJIWA KUJENGWA KITUO CHA AFYA KATIKA KIJIJI CHA
KIPANGANI SHEHIA YA KIFUNDI ILI ENEO
LITAKAYOBAKI LITUMIKE KWA SHUGHULI NYENGINE ZA KIJAMII.
AMESEMA NI VYEMA UONGOZI WA HALMASHAURI YA WILAYA
HIYO KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA ARDHI KUHARAKISHA UPIMANI WA ENEO LILILOTENGWA
KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA FYA CHA DARAJA LA PILI ILI UJENZI UANZE NA
UKAMILIKE KWA WAKATI ULIOPANGWA.
AKIZUNGUMZA
BAADA YA KULITEMBELEA ENEO AMBALO LINATARAJIWA KUJENGWA KITUO HICHO , MKUU WA
WILAYA AMEWATAKA WANANCHI WALIOANZISHA UJENZI WA NYUMBA NA KUISHI KUSIMAMISHA
UJENZI HADI PALE ZOEZI LA UPIMAJI LITAKAPOFANYIKA .
NAYE KATIBU
TAWALA MKOA WA KASKAZINI PEMBA AHMED KHALID ABDALLA AMESEMA
UJENZI WA KITUO HICHO ITAKUWA NI UKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI HICHO
KWANI KITUO CHA AFYA ZA SASA HAKITOSHELEZI KUTOA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO .
AIDHA AMEWATAKA
WAKAAZI WA KIJIJI HICHO KUENDELELE KUINGA MKONO SERIKALI KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUIMARISHA HUDUMA
MUHIMU ZA KIJAMII IKIWEMO AFYA NA ELIMU .
NAO WANANCHI
WA KIJIJI HICHO WAMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA WATENDAJI WA WIZARA YA AFYA WAKATI WA
UTEKELEZAJI WA KAZI ZA UJENZI IKIWA NI PAMOJA NA ULINZI WA VIFAA AMBAVYO
VITATUMIKA .
Post a Comment