Header Ads

Wananchi Shehia ya Kifundi Kaskazin Pemba Waipongeza SMZ

Related image 
MKOA WA KASKAZINI –PEMBA ……
WANANCHI WA KIJIJI CHA KIPANGANI SHEHIA YA KIFUNDI WAMEPOGEZA UWAMUZI WA SERIKALI WA KUTAKA KUWAJENGEAKITUO CHA AFYA CHA DARAJA LA PILI KATIKA KIJI CHAO NA KUSEMA KWAMBA KITAWAPUNGUZIA USUMBUFU WA KUFUATA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO KATIKA KITUO CHA AFYA CHA KONDE.

AKIZUNGHUMZA KWA NIABA YA WANANCHI WA KIJIJI HICHO RAMADHAN YUSUF  BAADA YA UONGOZI WA SERIKALI YA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KUTEMBELEA NA KUKAGUA ENEO AMBALO LINATARAJIWA KUJENGWA KITUO HICHO 

NAYE KATIBU TAWALA MKOA WA KASKAZINI PEMBA AHMED KHALID ABDALLA AMESEMA  UJENZI WA KITUO HICHO ITAKUWA NI UKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI HICHO KWANI KITUO CHA AFYA ZA SASA HAKITOSHELEZI MAHITAJI YA WANANCHI .

AFISA MDHAMINI WIZARA YA AFYA PEMBA BAKAR ALI BAKAR AMEWATAKA WANANCHI WA KIJIJI CHA KIPANGANI KUTOA USHIRIKIANO KWA MAFUNDI WAKATI UTEKELEZAJI WA UJENZI WA KITUO HICHO UTAKAPOANZA IKIWA NI PAMOJA NA KUVILINDA VIFAA AMBAVYO VITAPELEKWA KWA AJILI YA UJENZI .

KWA UPANDE WAKE MKUU WA WILAYA YA MICHEWENI SALAMA MBAROUK KHATIBAMEIOMBA  HALMASHAURI YA WILAYA YA MICHEWENI KUSIMAMIA UPIMAJI WA ENEO HILO ILI  MAENEO YATAKAYOBAKI YATUMIKE KWA SHUGHULI NYENGINE ZA KIJAMII.

No comments