DC MICHEWENI: Ni Marufuku Kusikia Mwanafunzi Kaozeshwa Kwenye Wilaya Yangu
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba Bi. Salama Khatibu Mbaruku, akizungumza na Walimu wakuu wa Sikuli za Sekondari Wilayani humo Ofisini Kwake Jana. |
mwalimu mkuu wa skuli ya Micheweni sekondari Ismail Ali, akimsikiliza kwa Makini Mkuu wa wilaya wakati wa Kikao Hicho |
Baadhi ya Walimu wakuu washiriki wakiendelea kumsikiliza Mkuu huyo wa Wilaya |
Walimu Wakuu wakishauriana Jambo na Mkuu wa Wilaya katika Kikao Hicho |
Na ali masoud
Walimu katika wilaya ya Micheweni wametakiwa kutowa ushirikiano katika kupambana na ndoa za mapema ili kuwapa nafasi wanafunzi kusoma masomo yao bila kuwa na vikwazo vya aina yeyote ile
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa wilya ya Micheweni Salama Khatibu Mbaruku wakati alipokuwa akizungumza na walimu wakuuu wa skuli za sekondari zilizopo wilayani humo
Amesema kuna wanajamii ambayo wanawaozesha waume wanafunzi na baadala yake kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu na kukosa wataalamu wa kike
Salama amesema ndoa za mapema na utoro ndicho kikwazo cha kukosa wataalamu wa ngazi mbali mbali ndani ya wilaya hiyo kuahidi suala hilo amelipiga sitopu
“tumejipanga katika wilaya yetu kuhakikisha mitihani yanayotarajiwa kufanyika hivi karibu wanafunzi ambao wameandikishwa wanafanya kikamilifu”alisema salama
Mkuu huyo wa wilaya amesema atapitia mashule yote yaliyomo wilayani humo ili kujuwa takuwimu za wanafunzi ambao wanahudhuria na wasio hudhuria ambao wote kupata masomo kama wengine
Hata hivyo mwalimu mkuu mtaaluma mkasha shame mbwana amesema wamefurahishwa na kitendo cha mkuu huyo wa wilaya kuwakumbusha wajibu wao ili kuweza kuisaidia jamii
Mkasha ameseama atahakikisha kuwa watakuwa wakibadilishana mawazo na walimu wazke ili kuhakisha watoro na wale ambao wanaolewa na kukatishwa masomo limefikia kikomo
Naye mwalimu mkuu wa skuli ya Micheweni sekondari Isimali ali ameseme wamejpanga kuhakikisha wanafunzi ambao wanatakiwa kufanya mitihani wanafanya yote bila kuwa na kikwazo cha aina yeyote ile
Post a Comment