Wazalendo Kujenga Mtaro wa Bubujiko Wete
Serikali Ya Mkoa Wa Kaskazini Pemba Imekutana Na
Wataalaamu Wa Ujenzi Ambao Ni Wazalendo Kujadili Ujenzi Wa Mtaro Ulioko
Bubujiko Wilaya Ya Wete Na Kuwataka Kuwa Wabunifu Na Watundu Na Kujiamini .
Akizungumza Kwenye Kikao Hicho Mkuu Wa Mkoa Wa
Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman Amesema Serikali Inaweza Kupunguza
Kutumia Gharama Kubwa Kufuata Wataalamu Kutoka Nje Ya Kisiwa Kazi Ambazo
Zinaweza Kufanaywa Na Wataalamu Wa Kizalendo .
Amesema Ni Vyema Wataalamu Wa Kizalendo Kupewa
Nafasi Ya Kuonesha Utaalamu Wao Na Kuwataka Wajumbe Na Wakuu Wa
Taasisi Zinazoguswa Na Ujenzi Wa Mtaro Huo Kuwatumia Wataalaamu Wa Kizalendo Na
Kuacha Kuwatumia Wataalamu Wa Kigeni Ambao Wanatumia Fedha Nyingi .
Naye Mkuu Wa Idara Ya Mipango Miji Pemba Abdalla Salim
Amesema Kamati za Kitaifa Na Kamisheni Ya Ardhi Zilifanya Kazi Ya Kukusanya
Data , Pamoja Na Kufanya Usanifu Kuutaka Uongozi Wa Baraza La Mji Wete
Kufuatilia Ili Kuona Hatua Ambazo Zimechukuliwa .
Post a Comment