DC Mkoani Apambana Kulinda Karafuu

Kikosi kazi cha
usimamizi wa ukoaji wa zao la karafuu kimempongeza Mkuu wa wilaya wa Mkoani na
kikosi kazi chake kwa kuendelea kusimamia vyema uokozi wa zao hilo
Kikosi hicho chini ya
mawaziri wasio na wizara maalum Mh Juma Ali Khatib na Mh Said Soud Said wamesema nia ya Serikali ni kuwalinda
wakulima na wachumaji kwa kuwasaidia
kukuza uchumi na kuondokana na umasikini wa kipato
Kwa nyakati tofauti
wameyasema hayo katika ziara yao ya kutembelea kambi na vituo vya kununulia
karafuu katika wilaya hiyo.
Mh Juma amesema katika
kuona kuwa lengo hilo linafanikiwa amewataka wazazi na walezi kutowaruhusu
watoto kuokota mpeta badala yake wawahimize kwenda skuli ili kuwaokoa na
vitendo viovu vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi yao.
Aidha waziri Said Soud Said amesema uchumaji katika
wilaya hiyo unaitia faraja Serikali kwa kuona unakwendana na ilani ya CCM ya
kuinua maisha ya wananchi wake na kuwataka kuunga mkono juhudi za Serikali
katika kuitunza rasilimali hiyo
Mapema Mkuu wa Wilaya
ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla amesema tokea uchumaji ulipoanza
wamefanikiwa kuwashajihisha wananchi
kuchuma na kuziuza karafuu zao katika shirika la ZSTC
Naye Mdhamini wa
Shirika la biashara la Taifa ZSTC Abdalla Ali Ussi amesema kwa ujumla wilaya ya
mkoani imenunua tani 1912 zenye thamani ya shilingi bilioni 26 za kitanzania.
Post a Comment