Header Ads

Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalumu Wawatembelea Wakulima Wa Karafuu Micheweni

Waziri asiokuwa na Wizara maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Juma Ali Khatib katika ziara ya kuwatembelea wakulima wa Karafuu Milaya Ya Micheweni kaskazini Pemba wakiwakagua walinzi wa ROAD BLOCK
Waziri asiokuwa na Wizara maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakizungumza na walinzi wa Karafuu-Tumbe, Kutoka Kulia Mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mh. Salama Mbaruku Khatibu
 


Waziri asiokuwa na Wizara maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Juma Ali Khatib akizungumza na wakulima wa karafuu


Msafara wa Mawaziri hao kuelekea kwenye mashamba ya karafuu

Baadhi ya Maafisa Kutoka Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Wakiendelea na Ziara hiyo

Waziri asiokuwa na Wizara maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Juma Ali Khatib Akishuhudia namna wakulima wanavyo dondoa Mpeta

Mkulima wa karafuu akidondoa Karafuu


MICHEWENI…………26/10
Wakulima wa zao la karafuu wilaya ya Micheweni wametakiwa kuuza karafuu zao shirika la biashara la taifa ZSTC ili serikali iweze kuwa na mapato zaidi kwa manufaa ya wananchi kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wasiokuwa na wizara maalum wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Juma Ali Khatib wakati katika muendelezo wa ziara maalum ya kuboresha zao la karafuu kisiwani pemba.

Amesema kuwepo kwa vituo vya kuuzia karafuu ni jitihada za serikali ili kuwarahisishia wananchi kuweza kuuza karafuu zao kiurahisi,na kuwataka kuweza kuvitumia vituo hivyo kama inavyotakiwa

Naye Said Soud amevitaka vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo vinashughulika na ulinzi wa zao hilo ikiwemo Road Block kuendelea kulisimamia zao hilo kwa ufanisi waweze kuliokoa zao hilo la taifa.

Aidha amemtaka afisa mdhamini ZSTC kuzishughulikia kero zinazowakabili walinzi hao kwa haraka

Naye mkuu wa wilaya ya Micheweni Salama Khatib Mbarouk amewashukuru mawaziri hao kwa kufanya ziara wilayani humo, na amewataka wananchi kuziweka karafuu katika sehemu salama hususani katika msimu huu wa mvua.

Ziara hiyo ya mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu wilaya ya Micheweni ni mwendelezo ya ziara ya mawaziri hao ya siku nne katika wilaya za kisiwa cha Pemba, ambapo wameweza kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.


No comments