Rais Dk. Shein Atumia Salamu Za Pongezi Kwa Wazambia
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu
za pongezi Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Changwa Lungu kwa kutimiza
miaka 53 tokea Taifa hilo kupata uhuru wake.
Salamu hizo zimeeleza
kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana pamoja na ndugu zao wa Zambia katika
kusherehekea siku hii muhimu katika historia ya nchi hiyo ambapo tukio hili la
kihistoria lilitokea Oktoba 24 mwaka 1964 ambapo Zambia ilipata uhuru kutoka
koloni la Kiengereza.
Aidha, salamu hizo,
zimeeleza kuwa tukio hilo kubwa, linatoa nafasi ya kuendeleza uhusiano na
ushirikiano mkubwa kati ya nchi mbili hizo hatua ambayo itaimarisha zaidi
uhusiano katika nyanja za Kitaifa na Kimataifa yakiwemo mashirikiano ndani ya
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU)
pamoja na Jumuiya nyenginezo za Maendeleo.
Sambamba na hayo, Dk.
Shein amemtakia kiongozi huyo pamoja na familia yake na wananchi wote wa
Jamhuri ya Zambia, afya njema na kuwatakia sherehe njema zenye amani na utulivu
wananchi wa nchi hiyo.
Post a Comment