Wazazi Kisiwani Pemba Waaswa Kuto Wasafisha Waathirika wa Udhalilishaji

WAZAZI na walezi
nchini, wametakiwa kutowasafisha watoto wao waliobakwa au kulawitiwa, na
ikitokezea wamewasafisha, wasisite kuwapeleka hospitali kuwafanyia uchunguuzi.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwendesha mashitaka kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kisiwani Pemba,
Mohamed Ali Juma wakati akijibu hoja za wajumbe wa kamati kuu ya mradi wa GEWE,
kwenye mkutano uliofanyika uwanja wa Gombani mjini Chakechake.
Amesema kukosekana kwa
maji maji maalum au mbegu za kiume kwenye sehemu iliofanyiwa tendo la ulawiti
au ubakaji, hakuuwi kesi, kama wengine wanavyofikiria, na wala ushahidi na
ubakaji haondolewi kwa kumuosha mtoto.
Mwendesha mashiataka
huyo, ameeleza kuwa hata kama wazazi au walezi watawaosha watoto wao,
waliobakwa au kulawitiwa chamsingi wawafikishe hospitalini, kwa ajili ya
kufanyiwa uchunguuzi wa kitaalamu, na iwapo wamebakwa njia zake za siri
zitaonyesha.
Kwa upande wake Afisa
Ustawi wa jamii wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed, amesema bado wasaidizi wa
sheria waliopo majimboni, hawajaibuka vya kutosha kushirikiana na wadau wengine
katika mapambano dhidi ya udhalilishaji.
Mratibu wa wanawake na
watoto shehia ya Kangagani Awena Salum Kombo, alisema lazima iwepo sheria madhubuti
ya kuwaadhibu, wasiotaka kufika mahakamani na kutoa ushahidi.
Post a Comment