Baba wa Kambo Adaiwa Kuwabaka Watoto Watatu Familia Moja KAS PEMBA
WATOTO watatu wa familia moja wamefanyiwa kitendo cha
udhalilishaji na baba yao wa kambo wenye umri wa miaka 8 , 14 na 16 huku mmoja kati yao akipata ujauzito .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi watoto hao wamesema
kwamba kabla ya kuanza kufanyiwa kitendo hicho na baba yao , alilazimika
kupandisha mizuka ambapo shetani aliwataka kuompinga anavyowambia baba yao .
Mmoja wa watoto hao amesema kwamba baada ya baba yao
kumfanyia kitendo hicho alimtaka kutomwambia mama yake na kuahidi kumfanyia
kitu kibaya iwapo atatoa taarifa hizo kwa mama yake au mtu mwengine wa karibu
yake.
Ameeleza chanzo cha kuanza mahusiano ya kimapenzi na baba
yake kilianza zamani na walikuwa wakifanya tendo hilo baada ya mama yake
kuondoka ambapo baba huyo alipata fursa ya kufanya naye tendo la ndoa.
Mama mzazi wa watoto hao (jina tunalo) akizungumza na
mwandishi wa habari hizi amesema kuwa , baada ya kumuona mwanawe amebadilika
kiafya na kumhoji iwapo naujauzito awali alikana na kudai yuko katika
hali yake ya kawaida .
Ameeleza kwamba hali ilimlazimu kumuita dada yake ili amuhoji
kwani mabadiliko kimwili dhidi ya mtoto
wake yalikuwa yanaonekana kwamba anaujauzito .
Amefahamisha baada ya kuhojiwa na mama yake mkuu , mshichana
huyo alikiri kuwa na ujauzito na kudai kwamba hakuna mwaname mwengine
aliyetembea naye isipokuwa baba yake ya kambo ambaye alikuwa akimlea.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishina Msaidizi wa Polisi Haji Khamis Haji amekiri
kuripotiwa kwa tukio hilo Ofisni kwake na kusema kwamba jeshi la polisi
linaendeela kumtafuta baba huyo ili aweze kufikishwa mahakamani .
Kamanda Haji
alifahamisha kwamba mtuhumiwa huyo anaendelea na kutafutwa na Jeshi la polisi
na akipatikana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili .
Naye mratibu wa wanawake na watoto kupitia mradi wa GAWE katika shehia hiyo Fatma Maulid Salim amesema
tukio hilo limemfanya ashirikiane na taasisi mbali mbali ili kudai haki ya
watoto hao .
Amesema pamoja na kazi wanayoifanya ya kuielimisha jamii
lakini bado baadhi ya wanajamii wanashindwa kutoa ushirikiano na hivyo
kusababisha badhi ya kesi kufanyiwa suluhu majumbani.
Kwa upande
wake sheha wa shehiya hiyo Omar Khamis Othman amewataka wananchi kuacha
kuyafanyia suluhu matendo ya udhalilishaji yanapotokea katika maeneo yao ili
wahusika waweze kuchukuliwa hatua kisheria.
Taarifa ambazo
zimepatikana na mwandishi wa habari hizi zinasema kwamba tayari mtuhumiwa huyo
amekamatwa na jeshi la polisi kisiwani Unguja na taratibu za kusafirishwa
kurejea Pemba kujibu tuhuma hizo .
Mwisho .
Post a Comment