DC MICHEWENI: Bado Siridhishwi na Mwenendo wa Utendaji Kazi wa Jeshi La Polisi
MICHEWENI 07/11/2017
Mkuu
wa wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib amewataka watendaji wa jeshi la
polisi wilayani humo kutekeleza wajibu na majukumu yao ipasavyo ili waweze
kuleta mabadiliko ndani ya wilaya hiyo.
Kauli
hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na wakuu wa vituo vya polisi viliomo
ndani ya wilaya hiyo kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya
mkuu wa wilaya ya Micheweni.
Amesema
haridhishwi na mwenendo wa utendaji wa vituo hivyo pamoja upokeaji wa kesi za
udhalilishaji, hivyo wakati sasa umefika kwa kila mmoja kufanya kazi ipasavyo
ili kukomesha matendo hayo.
Bi
salama amesema wilaya ya Micheweni inatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na wilaya
nyengine dhidi ya mapandano na watendaji wa matendo hayo na kuahidi kuwachukulia
hatua kali za kisheria ambao watasababisha kukwama kwa kesi hizo.
Kwa
upande wake mkuu wa kituo cha polisi Micheweni Koplo Khatib Sauti amesema kesi
15 za udhalilishaji zimeripotiwa kituoni hapo kuanzia Januari hadi Novemba
mwaka huu na kesi nne ndio ambazo zimeshapelekwa mahakamani.
Amesema
jamii bado haijakuwa na muamko wa haraka wa kuripoti kesi hizo pale tu
zinapotokea na badala yake huripoti kesi hizo baada ya wiki moja na zaidi jambo
ambalo linapelekea watuhumiwa kukimbia.
Post a Comment