Jamii Acheni Kuwaficha Majumbani Watu Wenye Ulemavu-DAWATI
MICHEWENI
Jamii imetakiwa kuacha kuwaficha majumbani watu wenye
ulemavu bali iwashirikishe katika kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo
katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa na afisa kutoka idara ya watu wenye
ulemavu kisiwani Pemba Mashavu Juma Mabruki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi
ya mkuu wa wilaya ya Micheweni wakati akiongoza mkutano wa siku moja
uliowashirikisha masheha wa wilaya hiyo wenye lengo la kupata uelewa wa zoezi
la usajili wa watu wenywe ulemavu.
Amesema zoezi la usajili wa watu wenye ulemavu ambalo
limeanza leo katika wilaya ya Micheweni linakwenda sambamba na haki za
binadamu.
Aidha amefahamisha kwamba kitendo cha kuwaficha watu
wenye ulemavu kinawanyima fursa ya kushiriki katika vikao vya maamuzi jambo
ambalo linawakosesha haki ya ushirikishwaji ndani ya jamii.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mwenyekiti wa masheha
hao Dawa Juma Mshindo amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili walemavu
ni pamoja na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji
Post a Comment