Halimashauri W/Micheweni Waagizwa Kushirikiana Maofisa Kilimo Kutatua Kero za Wakulima
Mkulima Said Sharif akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum SMZ, Shamata Shaame Hamis wakati wa Ziara ya Kulitembelea Shamba lake. |
Mkulima Said Sharif Akiwaonesha Viongozi hao baadhi ya Nanasi kati ya 4000, alizokwisha zivuna tayari kwa kupelekwa Sokoni |
Mkulima Said Sharif akitoa maelezo kwa viongozi hao namna ambavyo anatunza Mbolea kwa ajiri ya kutunza Migomba |
Na Gaspary Charles
Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum SMZ, Shamata Shaame Hamis amemuagiza Mkurugezi wa Halimashauri ya wilaya ya Micheweni Hamad Mbwana Shehe kushirikiana na maofisa kilimo kuwainua wakulima wilayani humo.
Naibu huyo ametoa agizo hilo mapema wiki hii katika ziara ya kikazi wilayani humo ya kukagua miradi mbalimbali kushudia namna wakulima wanaendesha shughuli zao.
Akiwa katika shamba la nguvu kazi lililopo Ruwi-Kinazini linalomilikiwa na mkulima Said Sharif, amemhakikishia mkulima huyo kuwa serikali itajitahidi kumsaidia kutatua changamoto zinazomkabili ili aweze kuendelea mbele zaidi.
Mkulima Sharif ametaja changamoto zinazomkalibili katika kuendesha shughuli zake za uzalishaji kuwa ni pamoja na kukosa Miundombinu rafiki ya maji kwaajiri ya umwagiliaji na Uhaba wa Mbolea kwani anazinunua kwa bei ghali.
Aidha katika hatua nyingine Naibu huyo ametoa wiki moja kwa mkurugenzi huyo kuhakikisha anawapatia vifaa waoteshaji wa Miche kitalo cha Kuotesha Miche ya Matunda na Misitu cha Wingwi Wilaya ya Micheweni.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Bi Salama Mbaruk Khatib ameahidi kwamba ofisi yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa wakulima wa wilaya hiyo kwa kuwapatia zana mbalimbali za kisasa.
Shamba la Nguvu kazi lenye jumla ya Ekari 3.7 linalomilikiwa na mkulima Said Sharif, linajumla ya Minazi 300, Miembe 100, Mifenesi 80, Miparachichi 70, Migomba 400, Nanasi, Vanila, Mihogo na Mazao mengine mbalimbali.
Post a Comment