Header Ads

ZAFELA Walia na Mikataba Umiliki wa Mali kwa Wanandoa Zanzibar



ndoaKutokuwepo  kwa Sheria Madhubuti  zinazosimamia  upatikanaji wa haki za wanawake kumekuwa kukirejesha nyuma  jitihada za wanawake wengi  katika  umiliki wa mali na kushindwa kujiendeleza kiuchumi.

Akizungumza na Jamii Fm radio Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria wanawake Zanzibar  ZAFELA,  Jamila  Mahmoud amesema  hali hiyo  inarejesha  nyuma  kwa wanawake kufikia malengo yao  kwani  sheria nyingi zilizopo  sasa ambazo  hazijatia mkazo mali za wanawake  hasa wakati wa ndoa  zinapovunjika.

Amesema  kesi  nyingi zinazopokelewa  katika Jumuiya hiyo zinatokana na  wanawake  wengi  kutokuwa na hati  maalum  ya umiliki wa mali pamoja na kuwepo  tabia ya kuaminiana bila ya maandishi kwa wanandoa.

Hivyo amesema  ili kukabiliana na tatizo  hilo Serikali  na Asasi za kiraia  hazinabudi  kutoa  elimu  maskulini na katika jamii juu ya  umuhimu wa kuwepo kwa mikataba ya umiliki wa mali kwa wanandoa.

Jumla ya kesi sita zilipokelewa  katika Jumuiya hiyo kuanzia mwaka jana hadi septemba  mwaka huu ambapo kesi tano zilifikishwa mahakaman na kesi moja imepatiwa usuluhishi.

No comments