Header Ads

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKABIDHI VIFAA VYA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI PEMBA



Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad Masauni akiwabidhi vifaa wakuu wa mikoa ya Pemba kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za polisi

 
Naibu waziri wa mambo ya ndani akiwa na wakuu wa Mikoa wa Pemba wakielekea kwenye meli ya Azam Sealink 2 kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya ujenzi wa nyumba za polisi
 
Naibu waziri akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za polisi kisiwani Pemba

PEMBA
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Hamad Masauni amewataka wananchi wa kisiwa cha pemba kuanchana  na siasa za chuki nabadala yake wayakubali nakuyaunga mkono maendeleo yanayoletwa na serekali kwa manufaa yao.
Masauni ameyasema hayo hukobandari ya Mkoani mkoa wa kusini Pemba alipokua akikabidhi vifaa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Polisi katika mikoa yote ya kisiwa cha Pemba.
Amesema Pemba ni miongoni mwa maeneo ambayo yamepewa kipaombele na wizara ya mambo ya ndani katika ujenzi wa nyumba hizo kutokana na askari wengi kuishi uraiani jambo ambalo linapelekea kutokua katika mazingira salama kwa askari hao.
Aidha amewataka wakuu wa mikoa yote ya Pemba kusimamia kwa ukamilifu ujenzi huo na kuunda kamati zitakazowashirikisha wananchi ambazo zitasimamia ujenzi wa nyumba hizo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ameshukuru kuletwa kwa mradi huo kwani ni Imani yake utapunguza tatizo la ukosefu wanyumba za Askari katika kisiwa cha pemba
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdallah ameahidi kusimamia kiukamilifu ujenzi wa nyumba hizo za polisi hadi zitakapokamilika na amewataka wadau wa maendeleo na wafadhili kujitokeza katika kuchangia uendelezaji wa mradi huo.
Vifaa vilivyo kabidhiwa katika hafla hiyo ni pamoja na Nondo, Saruji, Mabati na Rangi vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 400 ambavyo vitatumika kujenga nyumba 12 zinazotarajiwa kuchukua askari 50.

No comments