Halmashauri W/Micheweni Yashauriwa Kuongeza Vyanzo vya Mapato
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Omar Issa Kombo (KULIA), akiendesha kikao cha Baraza la Madiwani, (KUSHOTO) ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hamad Mbwana Shehe |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Hamad Mbwana Shehe, akiwasilisha Ajenda kwenye kikao cha Baraza la Madiwani |
Madiwani wakipitia Ripoti za kamati mbalimbali zilizowasilishwa kwaajiri ya mjadala katika kikao hicho |
Diwani wa wadi ya konde ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya mazingira, mipango miji na vijiji akichangia mada katika kikao hicho |
Mkuu wa wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib akipitia na kuandika maoni ya kamati mbalimbali za madiwani. |
MICHEWENI
Jumla ya milioni 32,802,613 zimetumika katika halmashauri
ya wilaya ya Micheweni katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo
ndani ya kipindi cha robo ya kwanza ya mwezi julai mpaka septemba mwaka huu.
Wakichangia katika
kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo, Diwani
wa wadi ya konde ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya mazingira, mipango miji
na vijiji, ameishauri halmashauri hiyo kuweka kituo cha maegesho ya magari
katika maeneo ya Micheweni na Konde kwani kwani ni sehemu mojawapo ya vyanzo
vipya vya mapato kama vitafanyiwa kazi.
Akijibu swali la Diwani
huyo juu ya gharama za tozo la mapato
kwa wamiliki wa magari ya abiria na mizigo, mkurugenzi wa halmashauri hiyo,
Hamad Mbwana Shehe, amesema kuwa kwa mjibu wa sheria halmashauri hutoza gari kiasi cha shilingi elfu 1,500 kwa kila tani
moja ya gari.
Aidha katika hatua
nyingine Mkurugenzi huyo amewaomba madiwani kutoa ushirikiano wa kutosha
kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo Kiwilaya inatarajia
kufanyika desemba 29 mwaka huu katika viwanja vya skuli ya secondary Micheweni.
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya Micheweni salama mbaruk khatib amewapongeza madiwani hao kwa ushiriki
wao kikamilifu katika kujadili vyanzo vya mapato ya halmashauri kwani
inamsaidia mkurugenzi katika kuratibu shughuli zake.
Mapema akiongoza kikao
hicho, diwani wa wadi ya Sizini Ambaye ni
mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, Omar Isa Kombo, amesema mapato hayo ni
chachu ya maendeleo
Post a Comment