Jibaba Miaka 56 ladaiwa Kumbaka Mtoto Miaka Tisa PEMBA
MKAZI wa Kangani Wilaya ya
Wete Mohammed Bakar Mshindo (56) , anatuhumiwa kumbaka mtoto wa wa kike mwenye
umri wa miaka tisa, huko katika nyumba
anayoishi Kangagani.
Wanafamilia wa mtoto huyo , walisema kuwa, mzee huyo alikuwa
akimchukuwa mtoto wao Skuli wakati wa mapunziko na
kwenda naye nyumbani kwake kumfanyia udhalilishaji.
Walisema kuwa, ni zaidi ya miezi miwili tokea kuripoti tukio hilo katika
kituo cha Polisi Mchangamdogo, ingawa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na
mtuhumiwa kujigamba kwamba yeye ni
mwenye pesa na hawezi kutiwa hatiani.
Akielezea tukio hilo mlezi wa mtoto huyo (60) alisema kuwa, mtoto
wake alitoka kwenda skuli na aliporudi akamuona hali yake sio ya kuridhisha,
ambapo alimuuliza kama anaumwa ampeleke hospitali.
“Aliniambia anaumwa na jipu na
ndipo nilipomwambia asiende skuli na nilimtafutia dawa ili ajipake, ingawa hali
ilizidi na kuwa mbaya na kutaka kumpeleka hospitali kwa siku ya pili”, alisema
mlezi huyo.
Alieleza kuwa, siku ya pili kabla
ya kupeleka hospitali alikwenda mazikoni na kupewa taarifa na mwalimu wake wa
darasa kwamba amekuwa na matumizi makubwa, jambo ambalo lilimshitua na kuanza
kumpeleleza kwani yeye alikuwa akimpa si zaidi ya shilingi 200.
Kwa upande wake mama mdogo wa
mtoto huyo (19) alieleza kuwa, walipomgundua mtoto wao siku aliyokwenda pwani
na watoto wenzake kuvua kaure, ambapo hakuweza kuokota kutokana na maji chumvi
kumuumiza sehemu alizoathirika.
“Aliporudi pwani hali yake ilikuwa mbaya hata kwenda alikuwa
hawezi na ndipo tulipotumia nguvu kumuangalia, tukamuona kwamba tayari
ameshaathirika”, alisema mama huyo.
Alieleza kuwa, walimuuliza aliyemfanyia kitendo hicho na kusema
kuwa ni Muhamadi Bakar Mshindo mkaazi wa Kangagani, ambaye alikuwa akimchukuwa
skuli wakati wa mapumziko na kwendanae, katika nyumba anayoishi na kumbaka.
Bibi wa mtoto huyo (40), alisema kuwa, baada ya kuwaeleza hivyo
walikwenda kituo cha Polisi Mchangamdogo, ingawa hadi leo haijachukuliwa hatua
yoyote ya kisheria kesi hiyo.
Nae mtoto (9) aliyefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, babu huyo
alimfanyia kitendo hicho mara mbili na alikuwa akimfunga matambara ya mdomo, pamoja
na kumuwekea panga kwa kumtishia ili asiseme.
“Alikuwa akinipa chipsi, pesa na akija skuli kunita wakati wa
mapumziko (rises) mimi na mjukuu wake, lakini siku aliyonibaka alinivuta ndani
na akaziba matambara na baadae mjukuu wake alikimbia”, alisema mtoto huyo.
Mratibu wa wanawake na watoto Shehia ya Kangagani Awena Salim
Kombo alieleza kuwa, kesi hiyo ipo kwa muda mrefu sasa na imeshafikishwa kituo
cha Polisi Mchangamdogo, ingawa hakuna chochote kilichoendelea zaidi ya
mtuhumiwa kupita mitaani na kujigamba.
Sheha wa shehia ya Mjiniole Khamis Shaaban Hamad alieleza kuwa,
pamoja na matukio ya udhalilishaji kutokea lakini wananchi wamehamasika
kuyaripoti kupitia elimu waliyopatiwa na mradi wa kukuza usawa wa kijinsia na
kuwawezesha wanawake GEWE.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Haji
Khamis Haji alisema kuwa, upelelezi wa kesi hiyo tayari umekamilika na tayari
jalada lishapelekwa kwa Mkurugenzi wa mashitaka.
Kamanda huyo alisema kuwa tukio hilo liliripotiwa Kituo cha Polisi
Mchanga mdogo Oktoba 13 mwaka huu, ingawa lilikaa mda mrefu kabla
halijaripotiwa na kuwataka wanajamii kuripoti kuharakisha kuripoti matukio
yanapotokea.
Jumla ya matukio manne yametokea ndani ya kipindi cha miezi miwili
katika shehia sita zilizopata elimu kupitia mradi wa GEWE, juu ya kuviripoti
vitendo vya udhalilishaji vinavyotokea katika jamii, ikiwemo Kangagani,
Mjiniole, Mchangamdogo, Kinyikani, Kiungoni na Shengejuu Wilaya ya Wete.
Na Masanja Mabula -PEMBA
Post a Comment