Header Ads

Utambulisho Unavyowakwamisha Waratibu Wa Shehia Kutekeleza Majukumu yao Micheweni

Image result for udhalilishaji


Waratibu wa shehia wanawake na watoto wilaya ya Micheweni wameiomba serikali ya mapibnduzi ya Zanzibar kuwapa kipaumbele ili kuepukana na changamoto zinazoweza kujitokeza dhidi yao.

Hayo wameyasema wakati walipokuwa wakizungumza na redio jamii Micheweni katika mahojiano maalumu na waratibu hao.

Mmoja wa waratibu hao, bi punje dawa juma amesema kuwa zipo changamoto kadhaa ambazo wamekuwa wakikutana nazo wakati wa ufuatiliaji wa kesi mbalimbali zinazojitokeza ndani ya jamii.

Akizitaja baadhi ya changamoto hizo amesema ni kama vile wakati wa ufuatiliaji wa kesi za udhalilishaji kutopatiwa ushirikiano kutoka kwa jamii kutokana na kutokuwa na utambulisho rasmi wa kuweza kuwatambulisha kwa jamii.

wameomba masheha kuwa msitari wa mbele kutoa ushirikiano kwa waratibu hao ili kuwatambulisha kwa wananchi ili wananchi wanapokuwa na tatizo wawe tayari kutoa ushirikiano kwa waratibu hao na kupatiwa ufumbuzi kwa matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika jamii.

 Waratibu wa shehia wameonekana kuwa na umuhimu zidi katika kutatua na kushighulikia kesi mbalimbali ndani ya jamii ambapo uwepo wao umesaidia kuibuliwa kwa matatizo yaliyokuwa hayalipotiwi kwa haraka katika vyombo husika.
 Micheweni
Na Time Hamis 

No comments