Waziri Aboud Aridhishwa na Utendaji Kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kas Pemba
Mkoa
Wa Kaskazini Pemba
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya
Makamo Wa Pili Mhe Mohammed Aboud Mohammed Ameelezea Kuridhishwa Na
Juhudi Zinazochukuliwa Na Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Kaskazini Pemba Juu Ya
Utekelezaji Wa Ujenzi Wa Mtaro Katika Eneo La Bubujiko Wilaya Ya Wete.
Akizungumza Baada Ya
Kutembelea Eneo Hilo , Mhe Abodu Amesema Ameutaka Uongozi Wa Serikali Ya Mkoa
Pamoja Na Wataalamu Wake Kushirikiana Na Wataalamu Kutoka Ofisi Ya Makamo Wa
Pili Ili Washauriane Na Kupata Ufanisi Wa Ujenzi Wa Mtaro Huo .
Amesema Kuwa Ni Bora Ujenzi
Wa Mtaro Huo Ukafanyika Haraka Ili Kuwakinga Wananchi Na Madhara Ambayo
Yanaweza Kuwapata Wananchi.
Mapema Katibu Tawala Mkoa
Wa Kaskazini Pemba Ahmed Khalid Abdalla Amesema Tayari Serikali Ya Mkoa
Imetayarisha Michoro Pamoja Na Kufanya Makisio Ambapo Zaidi Ya Shilingi Milioni
50 Zinatarajia Kutumika Katika Ujenzi Wa Mtaro Huo Wenye Urefu Wa Mita 200.
Amesema Tayari Timu Ya
Wataalamu Kutoka Wizara Ya Kilimo , Mawasiliano Na Ardhi Wameanza Mikakati Ya
Kuhakikisha Mtaro Huo Unajengwa Na Unakamilika Kwa Wakati .
Post a Comment