Kesi 112 za Udhalilishaji Mkoa wa Kaskazini Pemba Zaripotiwa
JUMLA YA
KESI 112 ZA MAKOSA YA UDHALILISHAJI WA
WANAWAKE NA WATOTO ZIMERIPOTIWA KATIKA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KWA KIPINDI
CHA KUANZIA MWEZI JUNAURI HADI OKTOBA MWAKA HUU .
Takwimu hizo
zimetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Omar Khamis Othman wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa
maagizo ya Mhe Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoyatoa wakati wa ziara yake
aliyoifanya katika mkoa huo Kisiwani Pemba .
Mkuu wa Mkoa amewashukuru wananchi waliojitokeza kutoa
taarifa juu ya matendo hayo na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na
serikali kuviripoti vitendo vya udhalilishaji
katika maeneo yao ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Mkuu
huyo wa Mkoa amewasisitiza wananchi kuacha kuyafumbia macho matendo hayo na badala
yake wayaripoti sehemu husika pindi yanapotokea katika maeneo yao .
Mapema Katibu Tawala Mkoa huo Amhed Khalid Abdalla
amesema utekelezaji wa maagizo ya Mhe Rais katika Mkoa huo yamekamilika kwa
asilimia kubwa kwani Serikali ya Mkoa kupitia vyombo vyake imeweza kusimamia na
kufuatilia hatua kwa hatua .
Hivyo amewataka
wananchi kushirikiana na Serikali kutunza miradi ambayo utekelezaji wake
umekamilika ili iweze kutumika kwa muda mrefu kwa manufaa ya umma.
Post a Comment