Header Ads

Usawa Kijinsia Siraha Pekee Kuiokoa Jamii ya Micheweni kwenye Janga la Udhalilishaji- Mwezeshaji Mafunzo UNESCO



Wazazi na walezi kisiwani pemba wametakiwa kufuata usawa wa kijinsia kwa watoto wao ili kujenga familia yenye usawa wa kinjinsia katika jamii.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Elimu ya Afya Wilaya ya Micheweni, Dk. Sulemani Faki Haji ambae pia ni mwezeshaji katika mafunzo hayo ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendelea katika Wilaya ya  Micheweni, Kas Pemba.

Amesema kuwa njia mojawapo ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa wa kijinsia katika jamii ni wazazi wenyewe kuzingatia kwanza usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa kuendelea kuwepo kwa mfumo dume katika jamii kwa kutowapa fursa sawa watoto wa kike kunaikosesha jamii na serikali kupata wataalam wa kike.

Mafunzo  ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendeshwa na UNESCO yanaendelea katika Skuli ya Sekondari Chwaka Tumbe ambayo yana lengo la kuunda Vikundi vya Vijana Shuleni na Akina Mama Watayarishaji Vipindi vya redio kwa kushirikiana na Redio Jamii Micheweni, ambavyo vitasambaza Elimu rika kwa Vijana na Akina Mama.

No comments