Walimu Madrasa, Wanafunzi watakiwa Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji
Sheha wa shehia ya
majenzi wilaya ya micheweni Faki Kombo Hamad amewataka wanafunzi pamoja na walimu wao kupiga vita vitendo vya
udhalilishaji pomoja na madawa ya kulevya.
Ameyasema hayo alipo kuwa akizungumza na walimu wa madrasa
mbalimbali na wanafunzi wao, kwenye chuo
cha Al-madrasat anuwari Imaniyah, juu ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hususani
kwa watoto.
Amesema walimu wamekuwa
wakidhaniwa kuwa nao wanachangia kwa kiasi Fulani vitendo vya udhalilishaji kwa
wanafunzi wao.
Katika hatua nyingine amewashauri
walimu hao kujua majukumu yao ndani ya madrasa zao ili kujiepusha na vitendo
vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanafunzi wao.
Nae kwa upande wake mjumbe
wa sheha wa shehia hiyo Ali Fundi Kombo amesema ni vyema wanafunzi kujua lengo
la kwenda madrasa na kuachana na vishawishi ambavyo vinaweza kuwapelekea
kudhalilishwa.
Kwa upande wa mwanafunzi
Faki Kombo Fundi amesema nivyema kuchukuliwa sheria kwa vijana ambao
wanawadhalilisha wazazi kwani suala la udhalilishaji haliko kwa mtoto wakike pekeyake.
Nae ustadhi Hamad Bakar
Hamad amesema lengo la mafunzo yanayotokana na madrasa hizo ni kukumbushana
mema na kukatazana mabaya vikiwemo vitendo vya nidhamu na udhalilishaji.
Post a Comment