Wananchi wilaya ya Micheweni Waaswa Kujikinga na Kipindupindu
Wananchi wa wilaya ya
Micheweni wametakiwa kuweka mazingira safi ili kujikinga na maradhi hatari ya
mripuko ya kipindupindu.
Kauli hiyo imetolewa na
mkuu wa wilaya ya Micheweni salama mbarouk khatibu wakati alipokuwa akizungumza
na wananchi wa wilaya ya Micheweni juu ya umuhimu wa kuweka mazingira safi.
Salama amesema maradhi
ya mripuko ya kipindupindu ni hatari ambayo yanaweza kuleta maafa makubwa ndani
ya jamii.
Mbarouk amesema ni vyema
wananchi kuweka utaratibu wa kuchemsha maji ya kunywa pamoja na kuweka mazingira
safi ili kujikinga na ugonjwa huo.
Hata hivyo amewataka
wananchi wa wilaya ya Micheweni kutomuonea haya mtu yeyote ambaye anafanya
uchafuzi wa mazingira katika wilaya yake.
Post a Comment