Bilioni 10 kutumika Kuimarisha Teknolojia ya Kisasa Sekta ya Nishati Zanzibar
Zaidi ya Shillingi Billioni kumi za kitanzania zinatarajiwa kutumika katika kuimarisha sekta za nishati ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi wa Zanzibar .
Akizungumza katika ufunguzi wa Semina ya siku tatu kwa lengo la
kuwajengea uwezo watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECCO ,Naibu
Waziri wa Ardhi , Maji , Nishati na Mazingira Juma Makungu Juma amesema
fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kununulia mita za tukuza
zitakazorahisisha upatikanaji wa mapato ya shirika na serikali.
Amesema utekelezaji wa mradi huo pia utawawezesha watendaji wa Shirika
ZECCO kuweza kujua namna ya kutoa huduma stahiki kwa wananchi pamoja
na kufanya kazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa itayoimarisha utendaji
wa kazi zao.
Aidha amewataka wasimamizi wa Mradi huo kufanya kazi kwa wakati na
kufuata sheria ili kuwaondoshea usumbufu wananchi wakati wanapohitaji
kufanya malipo.
Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Shirika la umeme Zanzibar ZECCO Salum
amesema kupitia Mradi wa SIDA unaotarajiwa kudumu kwa miaka mitatu
kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 utakao wawezesha kujifunza mambo mengi
katika ufungaji wa mita zinazoendana na kasi ya teknolojia.
Semina hiyo ya siku moja kwa watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar
ZECCO wakiwemo Wajumbe wa Bodi pia inatarajiwa kudumu kwa muda wa siku
tatu ambapo itawashirikisha Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati
Maji na Mafuta ZURA na Idara ya Nishati na Madini ili kuwajengea uwezo
katika kutekeleza majukumu yao.
Post a Comment