Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, Shirikisho la Wafanyakazi Zanzibar laitaka SMZ kujipanga Kikamilifu
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la wafanyakazi Zanzibar Khamis Mwinyi
Mohammed ameitaka Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba , kujipanga kwa ajili ya
kufanikisha sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi .
Amesema ni vyema Uongozi wa Serikali hiyo kuanza kuwahamasisha
wakuu wa taasisi za Serikali na binafsi ili waweze kushiriki katika maadhimisho
hayo ambayo kwa mwaka 2018 yanatarajia kufanyika mkoa huo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na uongozi wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama Mkoa huo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa kwenye kikao cha kujadili na kupanga mikakati ya kufanikisha
sherehe hizo .
Aidha ameshauri kuundwe kamati ambazo zitakuwa na jukumu la
kusimamia na kuratibu maandalizi ya sherehe ambayo mgeni rasmi anatarajia kuwa
ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohammed Shein
.
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa huo Mhe Omar
Khamis Othman amepongeza uwamuzi wa Shirikisho la wafanyakazi Zanzibar kwa
kuchagua mkoa huo kuwa mwenyeji wa kilele cha mei mosi.
Amesema Serikali ya Mkoa kupitia vyombo vyake vya ulinzi na
usalama itahakikisha amani na utulivu unakuwepo muda wote wa maadhimisho ya
sherehe hizo.
Post a Comment