Header Ads

Kijana Miaka 20 Wilaya ya Micheweni Apelekwa Rumande kwa Tuhuma za Kumbaka Punguani


Related imageMAHAKAMA ya Wilaya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, imempeleka rumande  kwa muda wa siku kumi na tatu kijana Ali Shangiti Juma (20) wa Micheweni   baada ya kufikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na tuhuma ya kumuinglia mwanamke punguwani .

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya , Mwendesha mashtaka kutoka Ofisi  ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali Mohammed Ali  ameiambia mahakama kuwa kijana huyo anadaiwa kutenda kosa hilo oktoba tano mwaka 2016.

Amesema siku ya tukio huko kataka msitu Mkuu Micheweni Ali Shangiti Juma  alimuingilia msichana  huku akijuwa kuwa ni mgonjwa  wa akili .

Baada ya kusomewa shitaka hilo  mtuhumiwa hakutakiwa kujibu lolote  kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za aina hiyo na kwamba kesi hiyo imepangwa kuendelea tena tarehe 29 mwezi huu katika mahakama ya Mkoa .

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka inaonyesha kwamba kijana huyo ametenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha 133 cha sheria ya kanuni na adhabu , sheria namba sita ya mwaka 2004 sheria za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments