Mkurugezi H/wialaya Micheweni asifia Utendaji Kazi wa Ilani ya CCM Wilayani humo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Hamad Mbwana Shehe (katikati), akizungumza na Wana kamati ya Shule ya Chimba Msingi wakati wa Ziara hiyo. |
Mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya Micheweni Hamad
Mbwana Shehe, amekishukuru Chama cha CCM kwa ngazi ya Wilaya kwa kuweza
kushirikiana na halimashauri hiyo katika kutatuwa kero za Wananchi Wilayani
humo.
Ametoa shukurani hizo katika ziara yake na viongozi wa Chama
hicho, wakati walipokuwa wakitembelea baadhi ya Skuli mbalimbali za Msingi na Sekondari
pamoja na Kituo cha Afya cha Mkia Ng’ombe ,ndani ya wilaya hiyo.
“Nakishukuru Chama cha CCM ngazi ya Wilaya kushirikiana nasi
kwa ajili ya kutatua kero za Wananchi na kuleta maendeleo katika masuala ya
afya pamoja na elimu hususa ni sehemu ambazo hazija patiwa huduma hizo”alisema.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Micheweni, Hassan Khatib Hassan, akikagua Ujenzi wa Shule ya Kisasa katika Jimbo la Micheweni |
Pia alisema lengo la ziara hiyo ni kwa ajili ya kuboresha
sekta ya Elimu pamoja na Afya na
kukabiliana na changamoto mbalimbali katika harakati za kimaendeleo ili
wananchi kuweza kupata huduma muhimu kwa urahisi.
Naye katibu wa CCM Wilaya ya Micheweni Hassan khatib Hassan
alisema lengo la Chama cha Mapinduzi ni kuhakikisha kinasikiliza kero
mbalimbali za wananchi na kushughulikiwa ipaswavyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Micheweni, Hassan Khatib Hassan, akisikiliza changamoto wanazozipata wakandarasi wa ujenzi wa Skuli hiyo ya kisasa |
Amesema Chama kimejipanga vyema kuwasaidia wananchi wote bila
ubaguzi wa itikadi za kisiasa na kuleta maendeleo kwa wananchi katika ngazi ya
wadi, jimbo na wilaya kwa ujumla.
“Chama cha CCM katika ilani yake imejipanga vyema kupeleka
mbele maendeleo ya Wazanzibar katika kila Wilaya hususa ni sehemu za vijijini
ili kuondoa kero mbalimbali za wananchi bili ya ubaguzi wa itikadi za
kisiasa”Hassan alisema.
Kwa upande wake
mwalimu mkuu wa Skuli ya Tumbe Sekondari
Nassoro Rashid Said amesema katika skuli hiyo wamekumbwa na changamoto
kubwa ya upungufu wa Madarasa pomoja na Walimu jambo ambalo linaleta usumbufu
skulini hapo.
Alisema Wanafunzi
katika Skuli hiyo wamekuwa wakichanganya madarasa mawili na kuwaweka katika
darasa moja ili kuweza kufundisha kutokana na tatizo hilo la Madarasa pamoja na
upungufu wa Walimu.
“Skuli yetu tatizo kubwa ni upungufu wa Madarasa pomoja na Walimu
jambo ambalo sisi walimu tumeamuwa kwa kila Darasa moja tuwachukuwe Wanafunzi
wa Madarasa mawili tuwaweke katika Darasa moja ili kupunguza tatizo
lililopo”alisema.
Naye daktari katika kituo cha afya cha mkia ng’ombe Hemed Abdallah
Ali ameiyomba Wizara ya afya ,chama cha CCM
ngazi ya wilaya pamoja na halimashauri ya wilaya kutoa msaada wa kuletewa
daktari atakae shuhulikia suala la kuzalishwa kwa mama wajawazito kituoni hapo.
Amesema katika shehia hiyo kumekuwa na usumbufu mkubwa katika
suala la usafiri kwa ajili ya kuwasafirisha mama wajawazito, kwa ajili ya
kwenda kujifungua sehemu nyengine.
“katika kituo hiki
tatizo kubwa ni akina Mama Wajawazito kuweza kufanyiwa msaada wakujifunguwa
hapa kituoni kwani sehemu kwa ajili ya kuzalishwa ipo isipokuwa hapana daktari
wa kulishuhulikia hilo ili suala la kujifungulia majumbani liweze
kuondoka”alisema Hemed.
Pia aliiyomba serekali msaada wa kuongewa Vyoo kwa ajili ya
kuondoa usumbufu wa kupanga msongo wa utumiaji wa Choo kwani katika kituo hicho
kina vyoo viwili na havikizi haja kutokana na watu kuwa wengi.
Katika ziara hiyo ya mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya na
katibu wa CCM wa wilaya wametembelea skuli ya tumbe sekondari, Skuli ya Chimba Msingi,
Skuli ya Mkia Ng’ombe Msingi na Kituo cha afya cha Mkia Ng’ombe.
Post a Comment