Header Ads

Tuhuma za Shambulio Mtoto wa Kike wa Miaka 3 na nusu zamtupa Rumande Mzee miaka 65 Wilani WETE KAS PEMBA

Related imageMzee hasan hamad faki 65 anayetuhumiwa na kosa la shambulio la aibu amepelekwa rumande na mahakama ya wilaya wete baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana .
Mzee huyo ambaye ni mkaazi wa Jadida anakabiliwa na kosa la kushambhulia kwa aibu mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mtatu na nusu , ametakiwa kuweka fedha taslimu shilingi milioni tatu na nusu .
Aidha masharti mengine ya dhamana ni kuwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja shilingi milioni mbili za maandishi .
Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali Mohammed Ali mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya kuwa  mtuhumiwa ametenda kosa hilo tahere 13/12/2017 majira ya tano za asubuhi.
Mtuhumiwa huyo amekana kutenda kosa hilo , ambapo ameiomba mahakama impe dhamana ombi ambalo limekubaliwa lakini ameshindwa kutumiza masharti ya dhamana na kupelekwa ryumande hadi tarehe 8/2/2018

No comments