Kamati ya Ulinzi na Uhifadhi wa Mtoto wilaya ya Micheweni yawataka Watoto wote walioacha Shule Kurejea Skuli
Wazazi na walezi katika
wilaya ya Micheweni wametakiwa kuwarejesha mara moja watoto wote waliocha shule
ili kuendelea na masomo yao kama kawaida.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na uhifadhi wa mtoto Wilayani hapa, Hamad
Othumani wakati akizungumza na watoto pamoja na wazazi hao katika ofsi ya mkuu
wa wilaya ya Micheweni.
Amesema wazazi
watakapokuwa mbele katika kusimamia masuala ya masomo kwa watoto wao, watoto
hao watakuwa na mwamko wa kupenda kusoma na kwenda shule kwa wakati bila
kukosa.
Hata hivyo kaimu afsa
elimu wilaya ya Micheweni Mwalimu Bakari Khamis amesema wamekuwa mstari wa
mbele kuwaelimisha walezi na wazazi juu ya kuwapatia watoto wao fursa ya kupata
elimu
Kwaupande wake mkuu wa
wilaya hiyo Salama Mbarouk khatib amesema hatamuonea haya mlezi au mzazi ambaye
atamkosesha mtoto wake haki yake ya msingi ya kupata elimu.
Amesema tayari wilaya
yake imekuwa ikipigania kuondosha ajira za watoto na watoto kutakiwa kurejea
shule ambapo tayari 300 wamerejea shuleni sasa toka kuanzisha zoezi hilo la
kuwarejesha shulebni.
Kwa upande wao wazazi na
walezi wameahidi kuwarejesha shule watoto na kuwasimamia ili kuweza kusoma na
baadala yake kupata wataalamu wa ngazi mbali mbali katika Taifa.
Post a Comment