Header Ads

'Wananchi Heshimuni Maeneo Tengefu kwaajiri ya Kujengwa Makaazi ya Waliopata Maafa wakati wa Nvua za Masika' Naibu Waziri Mh. Mihayo Juma

Image result for SMZ 
Naibu waziri ofisi ya makamo wa pili wa raisi, mhe. Mihayo Juma Nhunga ameshtushwa na  uvamizi wa eneo liliotengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wananchi walioathirika na mvua za masika .
 Akizungumza katika ziara yake ya kukagua  moja ya eneo ambalo linalotarajiwa kujengwa nyumba za wananchi walioathirika na mvua katika shehia ya Finya wilaya ya Wete , ameitaka serikali ya wilaya kuyalinda maeneo hayo ili yasivamiwe na wananchi kwa ajili ya makaazi na kilimo .
Mh, Nhunga amesema  wananchi wanapaswa kuyaheshimu maeneo ya serikali ambayo yamekusudiwa kujengwa nyumba za makaazi kwa wananchi waliopata maafa wakati wa mvua za masika mwaka uliopita .
 Nae mkuu wa wilaya ya wete  ndg  Abeid Juma Ali amesema serikali itachukua hatua kwa wananchi waliojenga katika eneo hilo bali watachukuliwa hatua kisheria .
 Amesema licha ua eneo hilo kuvamiwa na wananchi , lakini inatambua kwamba ni maeneo ya eka hivyo hitasita kuyarejesha  mikononi mwake.

No comments